Friday, June 14, 2013

*REDD'S MISS KINONDONI 2013 KUFANYIKA KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP JIJINI DAR


Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, ambapo alisema kuwa mwaka huu shindano hilo limeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.
Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. 
 Warembo hao wakipozi kwa picha....
Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000 pamoja na fedha taslimu tshs. 500,000.
Mshindi wa pili;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.
Mshindi wa tatu;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.

No comments:

Post a Comment