Thursday, June 20, 2013

* REDDS MISS KINONDONI TALENT 2013, KUPATIKANA LEO SHEKINAH GARDEN MBEZI BEACH


Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont, jijini Dar es Salaam. Kutoka (kushoto) kwa Albert ni Katibu Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta, wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano hayo Dennis Ssebo.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega, akizungumza na warembo wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 wakati Kamati hiyo, ilipowatembelea kambini kwao. Lundenga aliwaasa washiriki hao kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika fainali yao.

Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi.
**********************************************
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
KAMATI ya Miss Tanzania, ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga, jana iliwatembelea warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013, katika kambi yao ili kujua maendeleo ya kambi hiyo kuelekea kinyang'anyiro hicho cha kuwania taji la Redd's Miss Kinondoni Talent linalofanyika  leo alhamisi katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandhishi wa habari hizi, mratibu wa shindano hilo, Dennis Ssebo alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika kesho Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, SufianMafoto Blog, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, , Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment