Friday, June 21, 2013

*WALIOTINGA FAINALI ZA REDDS MISS KINONDONI TALENT NI SOPHIA, PHILLIOUS NA LINDA , KUCHUANA LEO KATIKA FAINALI ZA REDDS MISS KINONDONI 2013 LEO GOLDEN TULIP HOTELI JIJINI DAR


Washindi wa Redds Miss Kinondoni Talent 2013, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka washindi na kutangazwa washindi kutoka (kulia) ni Sophia Yusuf, Phillious Lemi na Linda Joseph.
Jaji mkuu wa shindano hilo, mtayarishaji wa Muziki, Man Walter akiwa na msaidizi wake wakati wa shindano hilo.
*************************************************
 Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
Washiriki watatu wamepatikana katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 lililofanyika katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Akitangaza washindi hao, jaji mkuu wa shindano hilo mtayarishaji wa Muziki, Man Walter, aliwataja washindi hao kuwa ni Sophia Yusuf, Phillious Lemi na Linda Joseph,  ambao waliibika kidedea baada ya kuwagalagaza washiriki wenzao 10 waliokuwa katika kinyang'anyiro hicho.
Naye Muandaaji wa shindano hilo, Dennis Ssebo, alisema kuwa fainali za mashindano hayo zinafanyika usiku wa leo katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata warembo bora watakaoiwakilisha nchi katika mshindano ya dunia.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Sufianimafoto Blog, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog. MATUKIO KAMILI YA SHOO HIYO BOFYA HAPO CHINI

No comments:

Post a Comment