Friday, June 21, 2013

*BEKI 'KISIKI' WA YANGA DAVID LUHENDE ACHUKUA NAFASI YA PAZI TAIFA STARS

Beki Kisiki wa Yanga, David Luhende (kulia) akiwa kazini.

Beki wa Yanga, Kisiki wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini TFF, Boniface Wambura, kwa niaba Kocha Kim Poulsen, alisema kuwa kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki wa kushoto wa Yanga, amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake, ambaye ni mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mechi ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).

Wengine ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar)

No comments:

Post a Comment