Saturday, June 15, 2013

* 'REST IN PEACE SHIDA' 'ANAKONDA' ALIVYOTESA WATU JANA, WENGINE WARUDIA GETINI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Jay Dee' A.K.A Komando Machozi, Anakonda, akiimba jukwaani na Mwana Hip Hop, Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye ni msanii wa siku nyingi, Joseph Mbilinyi, Mr ii, wakati wa shoo ya Anakonda ya kusherehekea miaka 13 ya lady Jay Dee iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Katika shoo hiyo, iliyokuwa ya aina yake, mashabiki kibao walishindwa kuingia ukumbini kumshuhudia mwanadada huyo kutokana na umati mkubwa wa watu waliofika ukumbini hapo na kushindwa kuingia baada ya ukumbini huo kujaa mashabiki kupita idadi iliyotabiliwa.

Msanii akicheza na nyoka.......

'Goo Bye Joto, Rest in Peace Shida', ni kama alitabiria mstari huo katika wimbo wake wa Joto Hasira, hapa akiokota mijihela aliyotunzwa na mashabiki wake wakati akishambulia jukwaa....
 Kimbembe kilikuwa hapa getini baada ya mashabiki lukuki kushindwa kuingia ukumbini humo, huku wengine wakiwa na tiketi zao mkononi

No comments:

Post a Comment