Tuesday, June 4, 2013

*BREAKING NEEEEWZ!! KIBANDA AWASILI NCHINI AAHIDI MAKUBWA KUHUSU TUKIO LAKE


 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo mchana akitokea nchini Afrika ya Kusini, alikokua akitibiwa. Baada ya kuwasili Kibanda, alizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia tukio lake huku akiahidi kuweka hadharani mkanda wa tukio zima.
 Kibanda, akilakiwa na Bosi wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari, Husein Bashe, pamoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali waliojitokeza kumpokea leo.
 Kibanda, akihojiwa na waandishi wa habari, baada ya kuwasili.
 Sehemu ya wananchi, Ndugu, Jamaa na Marafiki waliojitokeza kumpokea, uwanjani hapo.
Sehemu ya waliomlaki.......
*****************************************
NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Absolom Kibanda, amewasili chini leo akitokea Afrika Kusini alikokwenda kufanyiwa 

matibabu, baada ya kujeruhiwa vibaya na majambazi.
Kibanda aliyewasili jana mchana katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alivamiwa vibaya na 

majambazi kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kutobolewa jicho la kushoto.
Baada ya kuwasili, Kibanda alizungumza na waandishi wa habari mbalimbali wa habari kwa muda mrefu, akiwashukuru 

wananchi kwa kumuombea hadi kupona.
Pia, aliahidi kuelezea tukio zima lilivyokuwa na kuongeza kuwa anataka kukomesha matukio kama hayo ambayo yamekuwa 

yakitokea kila mara hapa nchini.
"Nawashukuru watanzania wote kwa kuniombea,serikali na wadau mbalimbali.Mungu akinijalia uzima nitaelezea tukio zina 

lilivyokuwa na pia naahidi kukosema matukio haya ya uovu ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa nchini." alisema 

Kibanda.
"Nataka matukio haya yasitokee tena na tukio langu liwe la mwisho," aliongeza Kibanda

No comments:

Post a Comment