Thursday, June 6, 2013

*KHADIJA KOPA AKISADIWA BAADA YA KUISHIWA NGUVU ALIPOPATA TAARIFA YA MSIBA WA MUMEWE AKIWA SAFARINI RUKWA

 Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto) akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa, baada ya kupata taarifa ya msiba wa mumewe,wakati akiwa kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda leo asubuhi. Mumewe alifariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri. Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana. 
Bi Khadija Kopa akisindikizwa kupanda ndege kurejea jijini Dar es Salaam.Picha na ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment