Friday, June 7, 2013

*JAPHET KASEBA APIMA UZITO LEO KUZICHAPA NA MMALAWI KESHO DDC KONDOA MAGOMENI

Bondia Japhet Kaseba, leo amepima uzito tayari kumkabili mpinzani wake Bondia, Rasco Chimwanza, kutoka nchini Malawi, katika pambano la Ubingwa wa Kimataifa.

Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony Ruta,Ibrahim Kamwe,Bondia wa kike, Pendo Njau na Dkt. John Lugambila wa hospitali ya Muhimbili.

Baada ya zoezi hilo, Dkt John, alisema kuwa Mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.

Kwa upande wake Kaseba, amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.

Katika pambano hilo la Kimataifa pia yatakuwepo mapambano ya utangulizi kati ya Juma Fundi atakayezichapa na Hassan Kiwale (Moro best), Joseph Onyango kutoka nchini Kenya atakayeonyeshana kazi na Seba Temba  wa Morogoro,huku Issa Omar- 'Peche Boy' atavaana na bondia mkongwe Juma Seleman na mapambano mengine mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa DDC Kondoa Magomeni.ddc magomeni kondoa 
 JUMA SELEMAN (digidigi au punch to punch) na bondia ISSA OMAR (peche boy) wakitunishiana misuli
Baadhi ya mabondia watakaopanga ulingoni kuonyesha uwezo wao hapo kesho

No comments:

Post a Comment