Sunday, June 9, 2013

*KASEBA BINGWA WA TAIFA WA PST AMGALAGAZA MMALAWI KWA KO RAUNDI YA TANO


 Bondia Japhet Kaseba (kulia) akichapana na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa pambano lao la Ubingwa wa Kimataifa wa PST lilliofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Kondoa Magomeni jijini Dar es salaam jana usiku. Katika pambao hilo,  Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano.
 Bondia Juma Fundi (kushoto) akichapana na Moro Best, katika pambano lao la utagulizi. Katika pambano hilo, Juma Fundi aliibuka na ushindi baada ya kumchapa kwa KO raundi ya sita.
 Bondia Ibrahimu Maokola (kushoto) akidundana na Joseph Njelekela. Maokola alishinda kwa KO ya raundi ya tatu.
Bondia Japhet Kaseba akiwa na mashabiki wake pamoja na mkanda wa Ubingwa wa PST baada ya kukabidhiwa mkanda huo jana alipomgalagaza Mmalawi kwa KO raundi ya tano.

No comments:

Post a Comment