Sunday, June 9, 2013

*SOMA RASIMU YA KATIBA MPYA HII HAPA KAMILI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika  Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
*********************************
KWA UFUPI 
Rasimu ya Katiba ina Ibara 240.

MISINGI:
uhuru, haki, udugu na amani

TUNU ZA TAIFA:
Utu,uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi uwajibikaji na lugha ya kiswahili,

-Mgombea Urais umri miaka 40,
-Kiwango cha kura za ushindi za urais ziwe zaidi ya asilimia 50,
-Matokeo ya urais kupingwa mahakamani (surpime cort).

MADARAKA YA RAIS:
-Kubaki kama yalivyo kwenye uteuzi wa viongoz wa ngaz za juu,
-Kushirikiana na taasisi nyingine,na kushauriwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuteua nafasi nyingine.

BUNGE,
-Bunge kuwa na madaraka ya kumshitaki Rais,
-Ukomo wa ubunge ni vipindi vitatu,
-wananchi kuwa na uwezo kumuondoa mbunge,
-Spika asiwe mbunge wala kiongoz wa chama cha siasa,

TUME YA UCHAGUZI,
-Kuitwa Tume Huru ya uchaguzi,
-wajumbe kuomba nafasi na kufanyiwa usaili na Kamati ya uteuzi,
-M/kt wa kamati ya uteuzi ni Jaji Mkuu,

MAHAKAMA;
-Kuunda suprime court (itakayosikiliza kesi za matokeo ya Uchaguzi nafasi ya Urais).

MUUNGANO;
Serikali tatu,
Mambo ya muungano yamepungua kutoka 22 hadi 7,

BUNGE LA MUUNGANO;
Mawaziri wasizidi 15,
Wabunge 70!
Hamna mahakama ya kadhi.

DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA
SURA
Rasimu ina Sura 15, ibara 130 na nyongeza tatu.
Sura ya kwanza inahusu Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na watu wake. uk. 1-4
Sura ya pili inahusu maadili na misingi mikuu ya taifa. uk. 5-7
Sura ya tatu inahusu haki kuu za binadamu na wajibu muhimu uk.7-21
Sura ya nne inahusu serikali ya shirikisho uk. 22-42
Sura ya tano inahusu Bunge la shirikisho uk. 43-63
Sura ya Sita inahusu mahakama kuu ya shirikisho uk. 64-67
Sura ya Saba inahusu Mahakama ya Rufani ya Shirikisho uk. 68-73
Sura ya nane inahusu vyombo vya dola vya Tanganyika na Zanzibar uk. 74-78
Sura ya Tisa inahusu sekretarieti ya Maadili uk. 79-80
Sura ya kumi inahusu masharti kuhusu fedha za Shirikisho uk. 81-88
Sura ya ya Kumi na moja inahusu madaraka ya umm auk. 88
Sura ya kumi na mbili inahusu majeshi ya ulinzi uk. 89
Sura ya kumi na tatu inahusu mamlaka ya kutunga katiba uk. 90-92
Sura ya Kumi na nne inahusu Tuma mbalimbali za taifa uk. 92-99 na
Sura ya kumi na tano inahusu mengineyo uk. 99-105
NYONGEZA:
Rasimu sifuri ina nyongeza tatu kama ifuatavyo:
(i) Nyongeza kuhusu mambo ya shirikisho
(ii) Nyongeza kuhusu mambo yasiyo ya shirikisho na
(iii) Nyongeza kuhusu idadi ya wizara za shirikisho
1
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA SHIRIKISHO YA TANZANIA NA WATU WAKE
TANGAZO LA JAMHURI
1. (1) Nchi yetu ni Tanzania na ni jamhuri ya shirikisho iliyoundwa kutokana na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na itaitwa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania;
(2) Eneo la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni eneo lote la Tanganyika na bahari yake pamoja na eneo lote la Zanzibar na bahari yake;
(3) Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi moja yenye dola moja na vyombo mbalimbali vya utekelezaji wa mamlaka ya dola;
(4) Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana.
WATU WA TANZANIA
2.(1) Uraia wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni wa kuzaliwa kwa wenyeji wa nchi na kuasilishwa kwa wageni;
(2) Wananchi wa Tanzania wataitwa Watanzania na watakuwa na haki ya uraia kwa mujibu wa Katiba hii na sheria zitakazotungwa na Bunge la Shirikisho la Tanzania kwa ajili hiyo;
(3) Watu wote waliokuwa raia wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1964 ni raia wa Tanzania;
(4) Mtu yeyote ambaye amezaliwa baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali wazazi wake wote wawili wakiwa raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania;
(5) Mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali mmoja wa wazazi wake ni raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania isipokuwa kama ataamua vinginevyo;
2
(6) Bunge laweza kutunga sheria itakayoweka masharti ya kuwawezesha watu wasiokuwa raia wa Tanzania kuwa raia kwa kuasilishwa.
DOLA YA KIDEMOKRASIA
3.(1) Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na haki za binadamu zilizotamkwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na katika Mkataba wa Haki za Binadamu na za Watu wa Umoja wa Afrika zitakuwa na nguvu za kisheria na zitachukuliwa kama ni sehemu ya Katiba hii.
(2) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania halitatunga sheria inayofuta au kupunguza nguvu haki za binadamu zilizoainishwa katika katiba hii, na mahakama zitafafanua na kufasiri haki hizo kwa kuzipatia nguvu kadri inavyowezekana badala ya kinyume chake;
(3) Sheria yoyote inayobadili masharti yanayogusa haki za binadamu zilizoainishwa katika katiba hii itapitishwa kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na kura zisizopungua theluthi mbili ya wabunge wote na kwa hali yoyote ile Bunge halitatunga sheria inayofuta mfumo wa vyama vingi vya siasa.
MFUMO WA SHIRIKISHO
4.(1) Utawala wa dola utafuata mfumo wa shirikisho utakaozingatia mgawanyo wa mamlaka ya dola kati ya mihimili mitatu yenye mamlaka ya utendaji, utoaji haki, na kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma;
(2) Muhimili wenye mamlaka ya utendaji utakuwa na Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
(3) Muhimili wenye mamlaka ya utoaji haki utakuwa na Mahakama Kuu ya Shirikisho, Mahakama Kuu ya Tanganyika, Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama ya 3
Rufani ya Shirikisho na vyombo vingine vya utoaji haki vitakavyoundwa kwa mujibu wa Katiba hii na sheria za nchi;
(4) Muhimili wenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma utakuwa na Bunge la Shirikisho, Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
MGAWANYO WA MADARAKA.SOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

No comments:

Post a Comment