Monday, June 10, 2013

MSANII WA MUZIKI WA BONGO FLAVER 'MATONYA' AFIKISHWA MAHAKAMA YA MWANZAO MKOANI RUVUMA KWA TUHUMA ZA UTAPELI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka jiji la Tanga, MATONYA, leo amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo mkoani Ruvuma kujibu shitaka la utapeli linalomkabili.

Msanii huyo amefikishwa Mahakamani hapo baada ya kudaiwa kutofika kufanya shoo aliyotakiwa kufanya kwenye ukumbi  wa Jambolee uliopo Manispaa ya Songea mkoani ruvuma. 

Imeelezwa kuwa msanii huyo alitinga ukumbini hapo akiwa hoi na hajitambui kutokana na 'Mitungi' yaani akiwa amelewa,  hali iliyompelekea kushindwa kufanya shoo hiyo na kusababisha hasara kubwa kwa waandaaji waliomualika baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbini hapo.

Baada ya tukio hilo, waandaaji wa waliamua kutangza kuahirishwa kwa shoo hiyo na kutangaza kuwa ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia, ili kufidia hasara hiyo.

Wakati waratibu wakitangaza hivyo, ilizuka varangati kubwa kwani msanii huyo alikuwa akipinga kurudia shoo siku ya pili yake kwani tayari alikuwa akitakiwa kupiga shoo nyingine siku hiyo ya pili Wilaya ya Mbinga.

Shoo hiyo ya siku ya pili ya Mbinga pia ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi na kusepa zake siku ya pili kurejea jijini Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo waandaaji walimfuata hadi alipo kuwa amefikia na kukuta amehamia sehemu nyingine. 

Waandaaji hao ilibidi kufanya kazi ya ziada ya kuwa 'Sungusungu' wa muda kwa kumvizia katika Kituo cha mabasi na ndipo walipomnasa na kumfikisha kituo cha polisi, ambapo leo ndiyo alifikishwa Mahakama ya Mwanzo

No comments:

Post a Comment