Monday, June 3, 2013

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN KUREJEA NCHINI LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia akiwa na ujumbe wake wakiangalia  Mazao ya Baharini Aina ya Chaza, mazao hayo  yakufuga yanaendelezwa na kampuni ya Peiyang Ablone, katika wilaya ya Xiang’an  iliyo katika mji wa Xiamen nchini  China,Rais na ujumbe wakiwa katika ziara ya mualiko wa Serikali ya Watu wa jamhuri hiyo. 
Mabwawa yaliyotengenezwa katika mpangilio maalum ya kufugia Mazao ya Baharini aina ya Chaza katika kampuni  kampuni ya Peiyang Ablone,katika wilaya ya Xiang’an  iliyo katika mji wa Xiamen nchini  China.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Jimbo la Xiamen Hong Chengzong, katika uwanja wa Ndege wa Mji huo Nchini china, akirejea Zanzibar baada ya kumalizika ziara yake nchini humo jana.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanammwema Shein,akiagana na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar Bibi Chen Qiman, katika uwanja wa Ndege wa Mji huo Nchini china,akirejea Zanzibar baada ya kumalizika ziara ya mualiko wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China jana. Picha na Ramadhan Othman Xiamen China

No comments:

Post a Comment