Monday, June 3, 2013

* CHUO CHA BIASHARA DAR (CBE) CHATWAA UBINGWA WA SAFARI LAGER POOL COMPITITION TAIFA


Mabingwa wa Pool 2013 timu ya Chuo cha Biashara jijini Dar es Salaam(CBE) wakishangilia na Kombe mara baada ya kukabidhiwa na Mwyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania,Dionis Malinzi yaliyofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya chuo cha CBE,Abukakar Amri  mara baada ya chuo hicho kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Lager Pool Competitio 2013yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Leadres jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi zawadi ya Bingwa wa Pool wanawake 2013,Liliana Meory kutoka chuo cha mara baada ya kuibuka Bingwa.
Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi zawadi ya mshindi wa Pool wanaume,Said Mohamed (kulia) wa Chuo Kikuu Ruaha (RUCO) mara baada ya kuibuka bingwa katika fainali hizo. Katikati ni meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
****************************************
Na Mwandishi Wetu.
CHUO kikuu cha Biashara(CBE), jana kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashidano ya mchezo wa pool Taifa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yakijulikana kwa 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013' baada ya kukifunga chuo kikuu cha Mzumbe Mbeya magoli 13-5 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Mashindano hayo  ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania(BMT), Dionis Malinzi, yalifanyikia kwenye  wa Viwanja vya Leaders Club mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Jumla ya vyuo vikuu vinane kutoka katika mikoa minane ambavyo vilipatikana baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa vilishiriki mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Vyuo hivyo ni Ruaha Universititi College (RUCO) kutoka Iringa, Mzumbe University(Mbeya Campus College) kutoka Mbeya,Mzumbe University-Morogoro,St.John University-Dodoma,Moshi University College of Co-operativeand Business Studies (MUCCOBS) kutoka Kilimanjaro,Institute of Accountancy Arusha(IAA) kutoka Arusha,mabingwa wa mwaka jana St.Augustine University of Tanzania (SAUT) kutoka Mwanza na wenyeji wa mashindano College of Business Education(CBE) ya Dar es Salaam
Chuo cha CBE kwa kutwaa ubingwa huo kwa mwaka 2013 kilijinyakulia Kombe na fedha taslim Sh.2,500,000 ambapo mshindi wa pili Mzumbe Mbeya kilizawadiwa fedha taslimu Sh.1,500,00.
Chuo cha Mzumbe Morogoro kilichukua nafasi ya tatu kwa kuwafunga mabingwa watetezi SAUT 13-8 na hivyo kujinyakulia fedha taslim Sh.1,300,000 na mshindi wa nne akawa SAUT ambaye alizawadiwa fedha taslim Sh.1,000,000.
Vyuo vinne vilivyotolewa kutoka katika mikoa mine ambavyo RUCO-Iringa,St.John Dodoma,MUCCOBS Kilimanjaro na IAA Arusha vilipewa kifuta jasho cha Sh.500,000 kila chuo.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Said Mohamed kutoka chuo cha RUCO Iringa aliibuka kuwa bingwa na kuzawadiwa fedha taslimu Sh.300,000  baada ya kumfunga George Titto wa SUA Morogoro ambaye ndiye mshindi wa pili alizawadiwa Sh.200,000.Mshindui wa tatu ni Patrick Peter kutoka chuo cha IFM ambaye alizawadiwa Sh.150,000 na wanne ni Walter Thomson wa TEKU Mbeya ambaye alizawadiwa Sh.100,000.
Udande wa wanawake, Lilian Meoli wa chuo cha CBE Dar es Salaam alifanikiwa kutwaa ubingwa na kujinyakulia fedha taslimu Sh.200,000 baada ya kumfunga Agnes Jacob wa chuo cha CBE Mwanza 2-0 ambapo Agnes alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa Sh.150,000.Mshindi wa tatu ni Amina Mhina wa chuo cha Mzumbe Mbeya alizawadiwa Sh.100,000 na wan ne Lemi Jaksoni kutoka St.Anthon Dodoma ambaye alizawadiwa Sh.50,000.
Kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania,Dionis Malinzi aliwapongeza wadhamini  wakuu wa mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza kuuinua mchezo huo na kuufikisha hapa ulipofika.
Malinzi pia aliwapongeza viongozi wa Chama cha Pool  kuanzia mikoa hadi taifa kwa ushirikiano  wao ambao umeendelea kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni vema mkaendeleza amani na ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool uendelee kumvutia kila Mtanzania.
Nakwa upande wa serikali inautambua kama ilivyo michezo mingine na Baraza la michezo itaendelea kuwaunga mkono katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze kuiletea heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa,"alisema Malinzi.

No comments:

Post a Comment