Wednesday, June 5, 2013

*TAMASHA LA ZIFF KUFANYIKA JUNI 29 HADI JULAI 7 MJINI ZANZIBAR


Mkuu wa masoko Wananchi Programming Bi. Wangeci Murage (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu. Katikati  ni  Mkurugenzi wa  Wananchi  Progamming ,  Bi. Hannelie   Bekker na kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF, Profesa Martin Mhando.
*******************************
Na Genofeva Matemu na Lorietha Laurence – MAELEZO
MAONESHO ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu.

Hayo  yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF Profesa Martin Mhando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo la 16 la kimataifa litakalohusisha nchi za Jahazi jijini Dar es Salaam.

 Alisema dhamira kuu ya tamasha hilo ni kuhakikisha kuwa ZIFF inaleta mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini  kwani imekuwa ikitoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wote na kuibua vipaji kwa kuzingatia kazi mbalimbali za sanaa na wasanii.

“Kupitia tamasha hili la 16 tunatarajia kutoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wa filamu mbalimbali na kuibua vipaji kwani mara nyingi tumekuwa tukifanikisha malengo ya wasanii mbalimbali na kuwawezesha kuwa wasanii mahiri katika tasnia ya filamu” amesema Prof. Mhando.

Naye Meneja Tamasha la ZIFF Bw. Daniel Nyalusi amesema kuwa tamasha limewahusisha watayarishaji wa filamu zaidi ya 35 mahiri kutoka nchi mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia ZIFF na kuwapa fursa hiyo maalumu kuongelea filamu zao na utengenezaji wa filamu kwa ujumla.

hapa nchini kuhudhuria kwa wingi na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wenzao toka nchi mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji vyao na kuweza kutoa filamu nzuri zitakazonyanyua soko la filamu hapa nyumbani.

“Miaka ya nyuma Tanzania hatukuwa na filamu nzuri katika soko la filamu hivyo kusababisha filamu za kinaijeria kuchukua nafasi kubwa na kuwafanya Watanzania wengi kufatilia filamu hizo ,lakini kwa kipindi hiki filamu zetu zimekuwa zikija juu kwa kasi kubwa sana hivyo kuua soko la filamu za kinaijeria kitu ambacho ni kizuri kwa taifa letu” amefafanua Bw. Nyalusi.

Alisema  katika maandalizi ya tamasha hilo linalohusisha nchi za Jahazi ZIFF lilihusisha filamu 257 toka nchi mbalimbali ambapo filamu 80 zilifanikiwa kuchaguliwa, kuoneshwa ili kuweza kushindania tuzo za ZIFF za mwaka huu.

No comments:

Post a Comment