Wednesday, June 5, 2013

DUUH! WABONGO NOMA WAJISEVIA NG'OMBE KATIKA AJALI.

 Lori lenye namba za usajiri T 382 BPE, likiwa limeangukia gari ndogo aina ya Vtz, lenye namba za usajiri T 685 BGZ, eneo la Mbezi Tangi Bovu, jijini Dar es Salaam jana usiku. Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa Lori hilo lilikuwa likijaribu kuipita gari hiyo ndogo na kupanda ukuta wa barabara na kukatika exel na kisha kuanguka na Ng'ombe wote waliokuwamo katika Lori hilo walitawanyika huku wananchi waliowahi kusogea eneo hilo wakianza kuswaga Ng'ombe kila mmoja akijisevia kwa wakati wake na njia yake na hadi Kamera ya Sufianimafoto inafika eneo la tukio walikuwa wamebakia Ng'ombe 5 tu huku wakizagaa zagaa katikati ya eneo la bustani la barabara hiyo.
 Hawa ndiyo Ng'ombe waliobaki kati ya waliokuwa wamejaa Lori hilo, hapa wakizagaa wasijue pa kwenda.
 Gari ndogo aina ya Vtz, likiwa limeegemewa na Loro hilo. Katika ajali hiyo Kondakta wa Lori alijeruhiwa lakini Dereva wa hili gari dogo, ambaye alikuwa ni mwanamke, alitoka mzima...............
 Baadhi ya mashuhuda wakishangaa ajali hiyo......
 Lori likiwa limeng'oka matairi baada ya ajali hiyo.....
Taswira ya ajali hiyo....

No comments:

Post a Comment