Thursday, June 6, 2013

*UKUMBI WA STEREO KINONDONI WATEKETEA KWA MOTO MCHANA HUU


 Gari la zimamoto likiwa eneo la tukio likizima moto ulioteketeza Ukumbi wa Stereo leo mchana. Mashuhuda wa liokuwepo eneo hilo walisema kuwa Moto huo ulioanza majira ya saa nane mchana umeelezwa kuwa umetokana na hitirafu ya umeme iliyoanza baada ya kutokea cheche za moto wakati mmoja wa wapambaji alipokuwa akiendele na kazi ya kupamba ukumbi huo kwa ajili ya sherehe iliyokuwa ifanyike ukumbini hapo leo jioni. 

Mashuhuda wengine walitonya kuwa baada ya moto huo Mtungi wa gesi uliokuwa jikoni pia uliripuka na kuongeza kasi ya moto huo. Aidha imeelezwa kuwa baada ya moto huo, gari la zimamoto liliwasili eneo la tukio baada ya dakika 20 ulipotokea moto huo lakini, liliondoka bila kufanya kazi hiyo ya kuzima moto baada ya kufika eneo hilo na kujikuta halina maji na hivyo likaondoka kwenda kujaza maji na kurejea tena.
 Hapa ni kwenye kona ya ukumbi huo kama inavyoonekana.
 Mamia ya wananchi wakishuhudia moto huo ukiteketeza ukumbi huo.
 Mmoja kati ya waliojitokeza kusaidia kuzima moto huo akimwaga maji ndani ya ukumbi huo kumalizia kuzima moto huo. Kwa picha zaidi bofya hapa chini

No comments:

Post a Comment