Thursday, June 6, 2013

*M To The P AWAHI KUMZIKA MSANII MWENZIE MANGWEA

Msanii Mgaza Pende a.k.a M2 The P, ambaye ameruhusiwa kutoka Hospitali hivi juzi alikokuwa amelazwa, nchini Afrika ya Kusini, amewasili nchini Tanzania na hivi sasa ameshafahamu kila kitu kuhusu kifo cha rafiki yake, Mangwea na tayari ameshwasili Mkoani Morogoro kuwahi kumzika rafike kipenzi.


hivi karibuni alitoka hospitali alikokua amelazwa Africa Kusini, amerudi Tanzania na yuko njiani kuelekea Morogoro kwa ajili ya kushiriki mazishi ya rafiki yake Albert “Ngwair” Mangwea leo.



Akihojiwa Live na kituo cha Redio Times Fm, leo asubuhi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Morogoro, M To The P , aliwashukuru Watanzania kwa kumuombea, ingawa bado hali yake 
haijarejea vizuri, alisema kuwa ameamua kurejea nchini ili aweze kumzika ndugu yake Mangwea.


Msanii M to the P akipita mbele ya jeneza la Msanii mwenzie Albert Mangwea aliyekuwa nae
mara ya mwisho kabla mauti hayajamfika


M 2 the P akilia kwa uchungu baada ya kupita mbele ya jeneza la Ngwea haamini kama kweli hatomuona tena rafiki yake kipenzi.


Jeneza lenye mwili wa Mangwea likishushwa kaburini.
bb21b674cea911e2918122000a9f4d8a_7
Hapa ndipo alipopumzika mpendwa wetu Albert Mangwea,Tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi
jina la Bwana lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment