Monday, June 3, 2013

*JICHO LA KAMERA YA MAFOTO NDANI YA JIJI LA DAR LEO


 Taswira ya jijini la Dar es Salaam kwa View ya juu, likionekana moja ya ghorofa linaloendelea kujengwa linaloelezwa kuwa huenda baada ya kukamilika likawa ndilo refu kuzidi majengo yote ya ghorofa jijini. Ghorofa hili lipo katika Barabara ya Kivukoni.
 Taa mpya za kuongozea magari katika makutano ya barabara ya Segerea na Ukonga, zikiwa tayari zimeanza kufanya kazi, huku daladala zikionekana kuendelea na vurugu zao za kufanya fujo kwa kutaka kupita pembeni hata bila kuruhusiwa. Kama inavyoonekana daladala hii pembeni kushoto.
 Hapa ni katika Barabara ya Bibi Titi, mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo mida ya asubuhi na jioni kuwa na foleni kama hivi.
 Hapa ni eneo la kutoka Kituo cha daladala cha Baridi kuelekea Kituo cha daladala cha Akiba, kona ya kuelekea Fire, ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea kwa kasi na hivi sasa kuanza kutoa Taswira mpya ya eneo hilo.
Hii ni moja kati ya Hoteli zilizokuwa maarufu sana jijini Dar es Salaam, Hotel Agip, ambayo kwa sasa inaonekana kutelekezwa huku eneo hilo likibaki kuwa eneo la wafanyabiashara wa Vitabu. Mbali na hoteli hii pia ipo Hoteli ya Embassy iliyopo Op na Supermarket ya Imaraseko, nayo pia inaonekana kutelekezwa na sasa ikionekana kuwa hifadhi ya walala nje....na huku ikiwa imezungushiwa mabati baada ya kuona kuwa ilikuwa imegeuka Naniliu Bubu ya watu fulani ambapo waliwahi kunaswa miaka ya nyuma eneo hilo.

No comments:

Post a Comment