Wednesday, June 5, 2013

*WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA NGWEA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KINONDONI VITUKO VYATAWALA


Wakazi wa jijini Dar es Salaam, leo wamejitokeza kwa wingi kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea, aliyefariki Mei 28, nchini Afrika ya Kusini. Mwili wa Mangwea  uliwasili nchini jana machana ambapo leo shughuli ya kuagwa mwili huo imekamilika majira ya saa saba mchana na kuanza safari ya kuelekea mjini Morogoro kwa maziko.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na wananchi mbalimbali, Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Wasanii wa filamu na baadhi ya Viongozi wa Serikali na wa Vyama vya Siasa.

Baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo, wananchi ambao asilimia kubwa waliokuwapo viwanjani hapo walikuwa ni vijana, walitoa kali ya mwaka pale walipomzonga msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond, kama nyuki wakati akiondoka viwanjani hapo na kuzua hofu kwa baadhi ya watu waliokuwapo eneo hilo wakizani lilikuwa ni tukio la hatari kutokana na jinsi kundi hilo la vijana lilivyokuwa likitawanyika kwa staili ya kutimka viwanjani hapo.

Msanii mwingine, aliyezongwa na vijana hao ni Mr. Blue, pamoja na Kitale, ambaye alizongwa hadi kuibiwa simu yake ya mkononi na kama ilivyo kawaida yake awapo katika Sini za Filamu, alimkamata mwizi wake na kumpakia katika gari lake na kuondoka naye kusikojulikana na kuwaacha watu hoi huku wakiangua vicheko na kuona kama alikuwa akiigiza.
Jeneza la mwili wa Mangwea, likiondolewa viwanjani hapo baada ya kuagwa.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Mangwea........
 P. Funky akipita kuaga na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Mangwea
 Wanafamilia wakipita kuaga mwili wa ndugu yao....
 Sehemu ya wanafamilia.....
 Huyu naye ambaye haikuweza kufahamika jina lake kwa haraka, akipiga picha huku akiangua kilio wakati wa kuaga mwili wa marehemu....

No comments:

Post a Comment