Monday, June 3, 2013

Mwli wa Marehemu Albert Mangwea kuwasili kesho saa Nane mchana baada ya kuagwa na wabongo South leo

 Jeneza lenye mwili wa Msanii Albert Mangwea likiwa katika eneo lililoandaliwa maalumu kwa shughuli za kuaga kabla ya kusafirishwa kureje nchini kesho majira ya saa nane machana na ndege ya South Africa Air Ways.
 Leo jioni watanzania waishio nchini Africa ya Kusini,  wamepata fursa ya kuaga mwili wa kipenzi chao, Marehemu Albert Mangweha kabla ya kusafirishwa kurejea nchini Tanzania kwa safari yake ya mwisho.
Pichani ni Baadhi ya watanzania waishio nchini Afrika ya Kusini wakiaga mwili wa Mangwea.

 Miongoni mwa wasanii waliokuwapo katika shughuli hiyo ni Msanii, wa muziki wa kizazi kipya, Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru ,Kinje, ambao ni wasimamizi wakuu wa shughuli za msiba huo. Kinje (katikati) akiwa na watanzania waishio nchini Afrika ya Kusini.
Msanii Bushoke kushoto, akiwa na mbongo mwenzake.

No comments:

Post a Comment