Sunday, June 9, 2013

*MKUU WA WILAYA YA SONGEA AENDELEA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANASIOFUATA TARATIBU NA KUHESHIMU MATUMIZI YA BARABARA


 Mkuu wa Wilaya Songea Ndg. Joseph Joseph Mkirikiti akiwapa maelekezo wafanya biashara ambao hufanya biashara zao kwa kupanga kandokando ya barabara kuu kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.
 Baada ya kupewa maelekezo na mkuu wa wilaya mama huyu ambaye hakufahamika jina lake kwa kuwa ni mwelewa  akaamua kukusanya bidhaa zake na kuelekea maaneo waliyotengewa kufanyia biashara zao ambayo ni Majengo
 Mkuu wa wilaya akiendelea kutoa somo kwa machinga ambao walikuwa upande wa pili kuwa si sahihi kufanya biashara maeneo hayo kwani ni hatari hasa kwa waendesha vyombo vya moto pamoja na watumiaji wengine wa barabara ambao baadhi huwa hawako makini wawapo barabarani .

No comments:

Post a Comment