Sunday, June 9, 2013

*UGANDA YAKARIBIA KUANZA KUNUSA SAFARI YA BRAZIL 2014, YAICHAPA LIBERIA 1-0 NYUMBANI


Timu ya Taifa ya Soka ya Uganda 'The Cranes', leo imeilaza Liberia bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Jijini Kampala, wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2014 zitakazofanyika Brazil,  na kuinua  matumaini ya mashabiki wake 

Kufuatia ushindi huo Uganda, sasa imepanda nafasi ya pili katika kundi J huku ikiwa na jumla ya alama 5 nyuma ya vinara wa kundi hilo Senegal ambao wanachuana na Angola.


Hadi sasa Uganda imesalia na mechi mbili huku ikishuka dimbani kukipiga na Angola Juni 15, mwaka huu, kabla ya kukutana na Senegal Septemba 6 mwaka huu katika uwanja wa Leopold Senghor.

Ili kujiweka katika nafasi nzuri ya matumaini, Uganda ni inatakiwa kushinda  mechi zake zote zilizosalia ili kujihakikishia safari ya Brazil 2014, zinazotarajia kuanza kutimua vumbi Januari mwakani.

Katika Kipute kingine cha kufuzu kwa Fainali hizo, Zambia wameilaza Lesotho kwa mabao 4-0,  huku Botswana wakielemewa nyumbani kwao na Ethiopia kwa kuchapwa mabao 2-1

No comments:

Post a Comment