Tuesday, June 17, 2014

BALIMI NGOMA FESTIVAL 2014"TABORA YASHINDA

Bw Robert Kaziwa (kushoto)akimkabidhi  mwakilishi wa wa kikundi cha Magereza Arts Group zawadi ya kitita cha Shilingi 600,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Balimi Kanda ya Ziwa ngazi za mikoa Mkoa Mkoa wa Tabora mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wacheza ngoma wa Magereza Arts Group wakishangilia na kitita cha Shilingi 600,000/=mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Balimi Ngoma Mkoa wa Tabora yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani humo.
Tabora,Shinyanga wapata mabingwa wa Balimi Ngoma.
Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili  ngazi ya mikoa zijulkanazo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Tabora na Shinyanga wamepata wawakilishi watakaowakilisha mikoa hiyo katika fainali za Kanda ya Ziwa zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014,  Mkoani Mwanza.
Mkoa wa Tabora kikundi cha Magereza Arts Group kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa huo na hivyokuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 600,000/= na tiketi ya kuwakilisha kwenye fainali za Kanda.Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Bugobogobo na hivyo kuzawadiwa  fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za Kanda.Jumla ya vikundi 8 ambavyo ni pamoja na JKT,Hekima,Uvikuja,Wembe Group,Hiari ya Moyo,Zugo Group.
Mkoa wa Shinyanga kikundi kilichofanikiwa kuchukua Ubingwa ni Mabulo ya Jeshi ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za Kanda.Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Wananguli Bugumbagu ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za Kanza Mkoani Mwanza.Jumla ya vikundi 10 Shinyanga vilishiliki ambavyo ni pamoja na Wagoyangi Bugumbagu,Buzori Usule,Bagoyangi Usule,Busumbi,Kadete Chibe,Wagoyangi Maswa,Wananguli Bugimbagu na Uswezi Usule.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager Fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba,  Musoma na Wenyeji wa mashindano Mwanza.

No comments:

Post a Comment