Tuesday, June 17, 2014

VIJANA WA KIMASAI WADUMISHA MILA NA DESTURI ZA KABILA LAO

Mgeni rasmi Mhe. Peter Toima Kiroya wa pili kushoto mkazi wa Manyara Wilayani Simanjiro ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akiwaongoza vijana wa kimasai kundi la Korianga kuingia kwenye boma kwa ajili ya kushiriki sherehe ya unywaji wa maziwa ikiwa ni mojawapo ya hatua ya makuzi kwa vijana jana mkoani Manyara, wapili kulia ni Mke wa Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya.
Mgeni rasmi Mhe. Peter Toima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akipokea Kibuyu cha maziwa kutoka kwa Mkewe Bi. Filomena Toima Kiroya kama ishara ya kuwaonyesha vijana waliohitimu hatua moja ya makuzi katika sherehe za unywaji wa maziwa Mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro.
Mmoja wa vijana wa kimasai kundi la Korianga akipokea kibuyu cha maziwa kutoka kwa mke wake kama ishara kuwa kuanzia sasa anaruhusiwa kunywa maziwa katika boma lake bila ya kujificha kama alivyokuwa akifanya kabla ya kuingia katika hatua hiyo ya makuzi kwa vijana wa kimasai.
Bw. Onesmo Toima akinywa maziwa yaliyomo katika kibuyu baada ya kuvuka hatua ya malezi iitwayo Sporio na kuingia hatua ya Korianga katika sherehe za unywaji wa maziwa zilizofanyika jana Mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa hotuba wakati wa Sherehe za unywaji wa maziwa kwa vijana wa kimasai kama hatua mojawapo ya malezi kwa vijana, kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga aliyekaa kulia katika picha ya pamoja na vijana wa kundi la Korianga, watatu kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na wapili kulia ni Mke wa Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya. (Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM)

No comments:

Post a Comment