Monday, June 16, 2014

SADIQ AL MAHDI AACHIWA HURU SUDAN.


Wakuu wa Sudan wamemuachilia huru kiongozi wa chama Kikuu cha upinzani, Sadiq al-Mahdi, ambaye alikamatwa mwezi uliopita kwa  mashitaka ya kuchochea chuki dhidi ya Taifa la Sudan.

Adhabu ya mashitaka hayo yanaweza kuwa kifo.

Bwana al Mahdi, ambaye anaongoza chama cha Umma, alilalamika juu ya sera za Serikali kuhusu Darfur na alishutumu wanajeshi wa  serikali kuwa wanakiuka haki za kibinaadamu, pamoja na ubakaji.

Waziri wa Habari wa Sudan, Yasser Youssef, alisema Sadiq al-Mahdi aliachiliwa huru kufuatia sheria za nchi, lakini hakueleza  kiundani zaidi kuhusu suala hilo.

No comments:

Post a Comment