Sunday, June 15, 2014

WANA NJIA PANDA WASHIRIKI KUFANYA USAFI HOSPITALI YA AMANA.

 Mtangazaji wa Kipindi cha Redio cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds FM Dkt. Isack Maro akizungumza na mwandishi wa habari wa Zanznbar Media Bi. Sophia Kingimali wakatika wa zoezi la usafi katika Hospilali ya Amana iliyopo Ilala, jana jijini Dar es Salaam. Wananjiapanda wamejitolea kufanya shughuli za usafi katika Hospitali hiyo ikiwa ni kutoa mchango wao kwa jamii inayowazunguka.
 Afisa Afya wa Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam Ally Kasembe akizungumza na mwandishi wa habari wa Zanznbar Media Bi. Sophia Kingimali wakatika wa zoezi la usafi katika Hospilali hiyo ambapo Wasikilizaji na wapenzi wa Kipindi cha Redio cha Njia Panda kinachorushwa hewani na Clouds FM walifika Hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya usafi wa mazingira yanayoizunguka Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Grace Products watengenezaji wa Vipodozi na bidhaa za usafi kwa kutumia mimea asili Bi. Happiness Tibaijuka akifafanu jambo kwa mwandishi wa habari Bi. Sophia Kingimali wakati wa zoezi la usafi wa Mazingira katika Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wana Njia Panda wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.

 Wana Njia Panda wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.

 Mmoja wa Wana Njia Panda Andrew Kwingwa kwa kushirikiana na Mfanya usafi wa kampuni ya Care Sanitation yenye jukumu la kufanya usafi katika Hospitali ya Amana, Bi. Anna Mkonda wakimwaka takataka katika jaa la kuhifadhi taka la Hospitali ya Aman kabla ya kupelekwa Dampo.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Grace Products watengenezaji wa Vipodozi na bidhaa za usafi kwa kutumia mimea asili Bi. Happiness Tibaijuka akikabidhi msaada kwa Afisa Afya wa Hospitali hiyo Bw. Ally Kasembe (kushoto).Grace Product wametoa msaada wa Sabuni za kuogea, mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto, sabuni za kusafishia choo, pamoja na Lotion.
 Wana Njia Panda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam jana.


Picha na Frank Shija, WHVM

No comments:

Post a Comment