Tuesday, June 17, 2014

UFALME WAMTAKA RAIS MUSEVEN KUOMBA MSAMAHA.

Mfalme Oyo
Ufalme wa kitamaduni wa Tooro nchini Uganda, umemtaka Rais wa Uganda Yoweri Museveni kumuomba msamaha mfalme wao na kuondoa matamshi yake ambapo alimuita mfalme huyo mtoto.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Uganda la The observer.
Jarida hilo liliripoti kuwa waziri mkuu wa ufalme wa Tooro, Minister Steven Kaliba, alionya ikiwa Rais Museveni hatoomba msamaha matokeo yake yatakuwa mabaya.
Hata hivyo waziri huyo amekanusha madai hayo.
Mfalme wa Tooro ana umri wa miaka 22 pekee na anajulikana kama Omukama Oyo. Rais Museveni alimuita mfalme huyo 'Akavuka ke Tooro' ikitafsiriwa kwa kiengereza kama kusema 'Kijana huyu wa Tooro.
Jarida la Observer limedai kuwa mfalme huyo anatishia kususia chakula kutokana na kile anachosema ni njama ya Rais Museveni kuvunja ufalme wa Tooro.
Mfalme Oyoo ni mfalme mdogo zaidi wa ufalme wa kijadi kwa Umri 
nchini Uganda
Ufalme hata hivyo, umekanusha madai hayo katika taarifa yake ukisema kuwa Mfalme huyo atafunga kula mwezi ujao kwa sababu za kitamaduni na kidini.
Ufalme umesema kuwa sio mara ya kwanza kwa mfalme wa Tooro na familia yake kufunga kukula , ukisema kuwa wao hufanya hivyo kila mwaka akitaka kumuomba Mungu kumpa mwongozo katika utawala wake.
Kadhalika ufalme huo umekana kuwa mfalme anafunga kula kwa sababu ya matatizo ambayo ufalme huo unakumbwa nayo.
Ufalme huo umesema kuwa umekasirishwa sana na matamshi ya Rais Museveni kumuita mfalme kama kijana ukisisitiza kuwa umri, rangi na muonekanao wa mfalme Oyo Nyimba Kabamba sio wa kuzungumziwa hadharani.
Licha ya kwamba kila mtu anaweza kutoa maoni yake kuhusu swala lolote, ufalme umetaka kumjulisha Museveni kuwa mfalme huyo ni fahari ya watu wa Tooro na kwamba awe mtoto au mtu mzima anajulikana tu kama mfalme.
Umemtaka Rais Museveni kukumbuka kuwa yeye ni mlinzi na kiongozi anayepaswa kutunzwa na jamii

No comments:

Post a Comment