Saturday, June 14, 2014

MAMA SALMA KIKWETE -MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA ILIYOFANYIKA KIGOMA.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya vifaa mbalimbali vinavyosambazwa na Bohari Kuu ya Madawa (MSD) huku akiwa ameshika mfuko wa damu wakati alipotembelea banda hilo katika uwanja wa Lake Tanganyika wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya wachangiaji damu duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Kigoma
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshuhudia Ndugu Mariam Juma,42, mkazi wa Shirika Mnarani huko Kigoma akitolewa damu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya waqchangiaji damu iliyofanyika kitaifa huko Kigoma tarehe leo. Katikati ni Ndugu Franco Mwikwa, Afisa mtoa damu salama kutoka ofisi ya Kanda ya Magharibi yenye makao yake makuu mjini Tabora.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa mji wa Kigoma walifika kwenye banda la kutolea damu wakiwa wanasubiri zamu yao kutoa damu wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama yaliyofanyika mjini humo


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa mji wa Kigoma waliokuwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kilele cha siku ya wachangiaji damu salama zilizofanyika kitaifa mjini hapo tarehe 14.6.2014. Wengine katika picha ni (kulia kwenda kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mheshimiwa Margareth Sitta, Mbunge na Mwisho ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Kabourou.
   Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakipita kwa furaha mbele ya mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani iliyoadhimishwa kitaifa huko Kigoma ambapo Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi.
 
 Wacheza ngoma kutoka wilaya ya Makamba nchini Burundi walioalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama wakicheza ngoma ya utamaduni  kwa umahiri mkubwa.

 Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama kitaifa Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenye uwanja wa Lake Tanganyika

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mfumo wa Kuhifadhi kumbukumbu za wachangiaji damu Tanzania  (Blood Establishment Computer system-BSCF) wakati wa Maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama duniani kwenye sherehe zilizofanyika kitaifa huko Kigoma
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo Ndugu Emmanuel Essay, Mfanyakazi wa KCMC inayotolewa na Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa mwanaume aliyechangia damu kuliko wote hapa nchini kwa mwaka 2013/14. Ndugu Essay ametoa damu mara 53 katika kipindi hicho.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa tuzo kwa Ndugu Restituta Mushi  kwa kuwa mwanamke aliyechangia kutoa damu salama kuliko wanawake wote hapa nchini katika mwaka2013/14. Restituta anatoka katika Mkoa wa Mwanza na ameweza kutoa damu mara 28 katika kipindi hicho.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kucheza pamoja na wananchi waliokuwa wakiwaburudisha wananchi wa Kigoma waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika

No comments:

Post a Comment