Tuesday, June 17, 2014

OKOCHA AMLAUMU KOCHA WA NIGERIA KWA MATOKEO MABAYA.

Jay -Jay Okocha
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Jay-Jay Okocha amemlaumu kocha wa timu hiyo kwa matokeo mabomu ya timu ya Nigeria iliyocheza dhidi ya Iran Jumatatu.
Timu hizo zilicheza mechi ya kwanza ya sare tasa katika michuano hiyo nchini Brazil.
"Keshi hakufanya kazi ya kutosha kuandaa timu. Mchezo wao haukufana hata kidogo Keshi anapaswa kuwajibika,'' aliongeza kusema Okocha"mechi hii ilipaswa kuwa ya ushindi wa Nigeria lakini hatukujitosa kimasomaso kushinda. Hatukufanya vyema , tulishindwa kabisa,'' alisema Okocha.
Mechi kati ya Nigeria na Iran haikuwa na msisimuko kama mechi zengina ambazo zimechezwa kufikia sasa.
Okocha, ambaye yuko kwenye kamati ya timu ya taifa ya Nigeria, alionekama kukosoa sana uamuzi wa Keshi kuhusu wachezaji walioshirikisha timu ya taifa.Alielezea kutofurahishwa, zaidi na kocha kwa hatua yake ya kumuondoa uwanjani mchezaji wa Liverpool,Victor Moses katika kipindi cha pili, na kumbadilisha na Shola Ameobi, ambaye aliondoka Newcastle msimu huu.
"Osaze (Peter Odemwingie) alikuwa na mchezo mzuri alipoingia uwanjani na tulihitaji acheze zaidi,'' alisema mchezaji huyo wa zamani.
Jonathan Akpoborie, ambaye ni mchezaji wa zamani, pia alihisi kuwa Super Eagles walikosa mwelekeo katika mchezo wao.
''Ninaamini kuwa pia tulipoteza mweleko katika mchezo wetu na tukaanza kucheza mipira ya mbali , mchezo ambao sio kawaida yetu, '' alisema Okocha
Mechi itakayofuata katika kundi F itachezwa Jumamosi dhidi ya Bosnia-Hercegovina, walioshindwa katika mechi yao ya ufunguzi kwa mabao 2-1

No comments:

Post a Comment