Tuesday, June 10, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO,ZINGA-BAGAMOYO.

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Shirika la International Health Partiners (IHP)-JEMA Tanzania, Mama Mary Ellen Kitundu mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo, mkoani Pwani. Mama Salma alikwenda kijijini hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la hospitali ya watoto inayojengwa na Shirika la IHP-JEMA Tanzania,Katikati ni Mkurugenzi wa Mradi huo Dkt. Jesse Kitundu.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi wakitembelea eneo linalojengwa hospitali ya watoto itakayo kuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 500 katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo 
 Baadhi ya wananchi kutoka katika kijiji cha Zinga na wageni waalikwa kwenye sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto wakifurahia jambo wakati mgeni rasmi Mama Salma Kikwete alipokuwa akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na wananchi wa Kijiji cha Zinga wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la hospitali ya watoto itakayokuwa na uwezo wa vitanda 500 

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto katika Kijiji cha Zinga huko wilayani Bagamoyo tarehe 10.6.2014. Kushoto kwa Mama Salma ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi.

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda mti kwenye eneo linalojengwa hospitali ya watoto katika kijiji cha Zinga wilayanI Bagamoyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi 

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, shirika la IHP-JEMA Tanzania na viongozi wa Kijiji cha Zinga mara baada ya sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto kijijini hapo leo.

No comments:

Post a Comment