Monday, June 16, 2014

RAIS AL SISI AMJULIA HALI MWANAMKE ALIYEONYESHWA KWENYE MKANDA WA VIDEO AKIBAKWA, YOUTUBE YAOMBWA KUONDOA PICHA MTANDAONI

Mwanamke aliyeonyeshwa kwenye kanda akibakwa atembelewa na Rais Al Sisi

Misri imeomba mtandao wa kijamii wa You Tube kuondoa video ya mwanamke akinyanyaswa kimapenzi katika mkutano wa kisiasa Cairo,kumuunga mkono rais aliyechaguliwa hivi majuzi.
Msemaji wa rais Abdul Fattah al-Sisi alisema ombi hilo lilitolewa na ubalozi wa Misri mjini Washington.
You tube bado haijaitikia ombi hilo la kuondoa kanda hiyo.Mwathiriwa alimuomba Bw.Sisi kuondoa video hiyo alipomtembelea hospitalini.
Video hiyo ambayo inaonyesha mwanamke akivuliwa nguo hadi kuwa uchi na kushambuliwa eneo la Tahrir square, ilienea mitandaoni mapema wiki hii.
Mfululizo wa mashambulizi wakati wa sherehe hizi za hivi majuzi yamelata vurumai.
Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali kilionyesha rais akiomba msamaha katika hospitali ya jeshi Cairo, kutoka kwa mwathiriwa ambaye hakutajwa.
Mwanamke huyo alionekana akimuomba Bw. Sisi kuondoa video hiyo ya matukio hayo kutoka kwa mtandao uliokuwa ukiisambaza.
"Mwanangu anazimia kila mara anapoiangalia,"alinukuliwa akisea mwanamke huyo.

No comments:

Post a Comment