Friday, June 13, 2014

WAKENYA WA NAKUMATI WAINUNUA MLIMANI CITY, WABONGO WAFURIKA KUNUNUA BIDHAA ZA PUNGUZO LA BEI

Makundi makubwa ya watu  yanaonekana yametapakaa katika eneo la shopping mall ya Shoprite ndani ya Mlimani City jijini Dar muda huu,baada ya Super Market mpya ya NAKUMAT iliyoinunua Shoprite kuamua kufanya SALE ya bidhaa mbalimbali zilizokuwepo kwenye Super Market hiyo,ili waweze uingia mzigo mpya. Pichani ni baadhi ya watu wakichangamkia SALE ya bidhaa hizo.
 Hili ni Nyomi linaloonekana kwa nje na ndani kuna idadi kuwa ya watu waliobahatika kuingia toka asubuhi,kwa ajili ya saula saula hiyo ya bidhaa.Milango ilifungwa kutokana na kutokea kwa vurugu kubwa la watu waliojitokeza kwa wingi kwenye Super Market hiyo.Mpaka sasa hakuna anaeruhuhusiwa kuingia.
 Wengine wameamua kukaa chini kusubiri kuona bahati iliwadondokea ya kuingia ndani ya Super Market hiyo kujipatia chochote kwa bei chee.

No comments:

Post a Comment