Friday, June 13, 2014

TANZIA: BONDIA WA ZAMANI IRAQ HUDU AFARIKI DUNIA LEO, KUZIKWA KESHO KISUTU DAR ES SALAAM.

Marehemu Iraq Hudu (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mwanae Daniel Hudu siku kijana wake huyu alipokula nondozzz yake katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Novemba mwaka jana.
Daniel na familia yake walikuwa katika maandalizi ya harusi aliyopanga kuifanya Juni 20, mwaka huu. Globu ya Jamii inatoa pole kwa wafiwa kwa msiba huu mzito. 
Iraq Hudu alikuwa mmoja wa wadau wetu wa karibu sana na Michuzi Blog ambapo yeye marehemu na nduguye Sensei Rumadha Fundi aliyeko Marekani alikuwa mshauri mkubwa wa kazi zetu. 
Mola Ipunzishe kwa amani roho ya marehemu peponi - Amin

BONDIA wa zamani wa ngumi za kulipwa nchini, Iraq Hudu 'Kimbuga' (49) amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo,  Dada wa Marehemu Tiba Takadiri, alisema kuwa Hudu amefariki jana majira ya saa 11 ya alfajiri kwenye hospitali ya Hindu Mandal, alikokuwa amelazwa. Takadiri, alimesema kuwa mazishi ya Hudu yatafanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
 Alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi, ambapo vilimsumbua kwa muda mchache kabla ya kufariki kwake. 
 "Marehemu alilazwa hospitali Hindu Mandal siku tatu zilizopita, ambapo majuzi jioni alizidiwa na jana asubuhi kukutwa na umauti", alisema Dada Tiba.
Hudu amezaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambapo alimaliza shule ya Sekondari na baadae kuanza shughuli za ngumi katika miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 alipoacha. 
 Marehemu ameacha watoto watatu, ambao ni Daniel alikuwa akitarajia kufunga ndoa Juni 20, wakati mtoto mwingine Msawila ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita. 
 Maandalizi ya msiba yanaendelea nyumbani kwa marehemu Buguruni Lozana Dar es Salaam ambapo kesho saa 7, atazikwa Kisutu. 
 Marehemu Hudu aliwahi kutamba akiwa na mabondia kina Joseph Marwa, Stanley Mabesi, na baadae wakaja mambondi wengine Rashid Matumla na Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo'. Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu amina..

No comments:

Post a Comment